Afariki Baada ya Kuchapwa na Wazee wa Kimila - FARMERCIST 254

FARMERCIST 254

This site discusses farming issues in relation to Kenya with particular emphasis on poultry farming.

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday 26 June 2016

Afariki Baada ya Kuchapwa na Wazee wa Kimila



Picha ya Tukio jingine
Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Kandashi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro, Abedi Akyo (53), amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchapwa viboko na wazee wa kimila kwa tuhuma ya kujihusisha na wizi wa kuku.

Akielezea mazingira ya kifo hicho, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilfred Mutafungwa amedai kuwa Akyo alichapwa viboko 70 na wazee hao wa kimila wa Kimeru na Kimasai.

Mutafungwa amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwezi uliopita  wakazi wa Kata ya Karansi wilayani hapa  walitoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages