Akiongea wiki hii, Harmozine amesema mpenzi wake huyo alionyesha nia ya kutaka kukujua ukweni na yeye akaona hakuna sababu ya kumbania.
“Mimi sijazaliwa pale Mtwara mjini, nimezaliwa Wilaya ya Tandahimba. Kwa hiyo wakati nataka kwenda kwenye show baby naye akataka kuja, nikaona pia ni kitu kizuri kwa kuwa anakuja pia kunisupport kwa sababu unajua uwepo wake ni kitu mihimu kwa kuwa ana mashabiki wengi, so nikivutio cha watu. Nikamwambia pia mimi natakiwa kwenda kijijini nikawasalimie wazazi, akasema kwanini tusiende wote, so tukaenda wote, familia yangu imemuona, imemjua na pia imempokea vizuri,” alisema Harmonize.
No comments:
Post a Comment