(PICHA:) Ukweli kuhusu mtoto wa mwaka 1 nchini India anaedaiwa kukua tofauti na binadamu wa kawaida huu hapa.. - FARMERCIST 254

FARMERCIST 254

This site discusses farming issues in relation to Kenya with particular emphasis on poultry farming.

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday 3 June 2016

(PICHA:) Ukweli kuhusu mtoto wa mwaka 1 nchini India anaedaiwa kukua tofauti na binadamu wa kawaida huu hapa..

Mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja nchini kutoka nchini India,anaefahamika kwa jina moja la Akash,anadaiwa kukua tofauti na ukuaji wa kawaida ambapo licha ya umri mdogo alionao tayari ameanza kuwa na hisia za kimapenzi ikiwa ni pamoja na kuota nywele kichwani na katika sehemu zake za siri,huku viungo vyake vya uzazi vikiwa sawa na vya mtu mzima. Kwa mujibu wa gazeti la Hindustan Times la nchini India,Mama mzazi wa mtoto huyo ambae jina lake halijawekwa wazi amedai kuwa baada ya kujifungua mapema mwezi July mwaka jana,mtoto wake alianza kukua kawaida ila kadri siku zilivyokwenda alianza kushuhudia mabadiliko ya ukuaji mtoto wake usio wa kawaida, “We th ought he was just a big baby but later everyone started to point out that that this growth couldn’t be normal,”.Alidai Mama wa mtoto huyo. Daktari anaemtibu mtoto huyo anaefahamika kama,Vaishkhi Rustagi amedai kuwa ukuaji wa aina hiyo kama ilivyo kwa Akash husababishwa na uvimbe kuwepo kwenye ubongo au tumboni hali inayopelekea uzalishaji mkubwa wa seli hai za mwili sambamba na ukuaji wa misuli ya mwili usio wa kawaida ambapo hufikia hatua mtu kuwa mkubwa kiasi kwamba hawezi kudhibitiwa tena.“Usually this disorder is caused due to brain or stomach tumour,muscle strength increased to a level that even his parents couldn’t control him,”.Alisema Daktari huyo. Wazazi wa Akash walimfikisha mtoto wao katika hospitali ya Super Max Specialist akiwa na miezi 18 huku sauti yake ikiwa sawa na ya mtu mzima mwenye umri wa miaka 25,ambapo licha ya kufanyiwa uchunguzi juu ya tatizo lake ambalo kitabibu linafahamika kama “precocious puberty”,Madaktari wamekua wakimpa dozi ya kudhibiti homoni na ukuaji wa misuli ya mwili ambapo matokeo ya dozi hiyo yataonekana baada ya miezi mitano. -VitukoVyaMtaa

For More Music Updates And News FIND US ON:

TWITTER: @MzukaKenya

FACEBOOK: Mzuka Media

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages