Nimeamua kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa wimbo mpya – Lady Jaydee. - FARMERCIST 254

FARMERCIST 254

This site discusses farming issues in relation to Kenya with particular emphasis on poultry farming.

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday 4 July 2016

Nimeamua kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa wimbo mpya – Lady Jaydee.

Msanii mkongwe wa muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amefunguka kwa kusema kuwa hataki tena kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia kazi. Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Sawa na Wao’ hivi karibuni, amekiambia kipindi cha East Africa Breakfast kinachoruka East Africa Radio kuwa anachofanya ni kutoa kazi moja moja kutoka katika albamu yake mpya iitwayo’Women’. “Unajua mimi nina marafiki mbalimbali wa rika zote, wapo walionizidi sana umri, wapo nalingana nao na wengine ni wadogo zangu kabisa hivyo muda mwingi napotoka nao au kujichanganya nao ndipo nikapata wazo la wimbo huu ‘Sawa na wao’ kwani binadamu tunatofautiana. Saizi nimeamua kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa kazi moja kutoka kwenye album yangu hiyo ya ‘Woman’,” alisema Lady Jaydee. Lady Jaydee amesema wazo la wimbo ‘Sawa na Wao’ ambao ameuachia hivi karibuni alilipata kutokana na maisha ya watu wake wa karibu ambao amekuwa akiishi nao katika maisha ya kila siku.

For More Music Updates And News FIND US ON:

TWITTER: @CelebTheKing

FACEBOOK: Celeb The King

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages