Belle 9 Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kujiunga WCB na Diamond Kuwa Msanii Mkubwa Afrika. - FARMERCIST 254

FARMERCIST 254

This site discusses farming issues in relation to Kenya with particular emphasis on poultry farming.

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, 27 August 2016

Belle 9 Afunguka Kuhusu Tetesi Za Kujiunga WCB na Diamond Kuwa Msanii Mkubwa Afrika.

Belle 9 amekana kusaini na WCB na kudai kuwa alienda kutembelea kwenye ofisi zao kwakuwa Diamond ni msanii mkubwa Afrika na amefanikiwa kufika mbali kimuziki. “Diamond ni msanii mkubwa Afrika ila Watanzania tumekuwa wagumu kulikubali hilo,” amekiambia kipindi cha E News cha EATV. Belle 9 aliongeza kuwa alienda WCB kwa ajili ya kuwatembelea na kufanya nao mazoezi kwa sababu anamheshimu Babutale kwakuwa ndiye aliyemkutanisha na menejimenti yake aliyonayo. Katika hatua nyingine, muimbaji huyo amesema kuwa bado ana mkataba na menejimenti yake hivyo hawezi kusaini mkataba kwingine labda mpaka utakapomalizika. Na kuhusu WCB amesema anaweza akasaini nao endapo wakikubaliana na mambo yakienda sawa.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages