Siku ya jumanne imeingia katika kumbukumbu za kihistoria nchini Kenya baada ya CEO wa Facebook kutua nchini ghafla. Mark Eliot Zuckerberg ambaye ni tajiri wa sita duniani ametua nchini kwa kushtukiza baada ya kutokea Nigeria. Inakuwa ni safari yake ya kwanza kuzuru bara la Afrika chini ya jangwa la Sahara kwa mujibu wa jasiriamali huyo mkubwa duniani. Zuckerberg mwenye umri wa miaka 32, alifika Lagos hii chini ya ulinzi mkali na kuzuru katika maeneo na vituo vya teknologia hump pasina mtu kufahamu. Aliweza kutangamana na mastaa wa muziki miongoni mwao Yemi Alade. Baada ya hapo alitua jiji la Nairobi Kenya Kama alivyokuwa ametangaza kupitia kwa mtandao kwa kuandika: “Just landed in Nairobi! I’m here to meet with entrepreneurs and developers, and to learn about mobile money — where Kenya is the world leader”. Ametangamana na watu wengi kwenye sekta ya biashara na ujasiriamali pamoja na kutembelea vituo vya ufundi na teknolojia ili kujifunza kuhusu mwenendo wa makampuni machanga. Amekuja kujifunza kuhusu mfumo wa kutuma na kusambaza pesa kwa kutumia simu na ambao ulianzishwa nchini Kenya. Zuckerbarg amezuru na kula Samaki kwa Ugali katika mgahawa wa mama wa mchezaji wa timu ya taifa, Oliech. Mgahawa huo ambao upo sehemu za Yaya Center, amekuwa pamoja na ICT Cabinet Secretary Joe Mucheru na Principal Secretary Victor Kyalo. Hii ni orodha ya mastaa na watu mashuhuri waliowahi kuzuru Kenya kimyakimya. 1. Bill Gates- Tajiri wa kwanza duniani. Alizuru mwaka 2009. 2. Jose Mourinho- Mkufunzi wa Manchester united. Alizuru mwaka 2012. 3. Naomi Campbell-British Super Star model. 4. Nicholas Cage- Mshindi wa tuzo ya Oscar. Alizuru mwaka 2014. 5. Alicia Keys- Mshindi wa tuzo za American Grammy. Ni mwanamuziki. Alizuru mwaka 2011.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Friday, 2 September 2016
Facebook CEO azuru Kenya ghafla
Tags
# News
Share This
About Farmercist
News
Labels:
News
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment