Wasafi walikuwa na show mbili mtawalia nchini Kenya. Wakali hawa ni pamoja na Raymond aka Rayvanny, Harmonize na Rich Mavoko. Walipokuwa mji wa Mombasa kulishudiwa tukio la aina yake wakati mkali huyu wa “Natafuta Kiki” alipomwaga moyo wake na kumwita jukwaani msanii mwanadada wa Kenya, Avril. Avril Kenya anafahmika kwa wimbo wake aliyomshirikisha AY “No Stress”. Rayvanny aliweka mambo kadamnasi kwa mashabiki kusema kuwa anampenda msanii huyo wa kike. Aliandika kwenye mtandao,” Trust me @theavieway I really love you… Thank you for coming.. God bless you ” aliandika Ray.
Kama haitoshi, Avril naye akasambaza picha yao pamoja na kuandika hivi, “This song that @rayvanny serenaded me with should be my next collabo.hmm #ThinkingOutLoud” Hivyo ni baaya ya mkali huyo wa freestyle kuita jukwaani na kumuimbia wimbo wake maalum kitu kilichofanya mashabiki wa shangilie hali hii. Avril baada ya kutoswa na mwenzake wa South Afrika atakuwa anafarijika kutokana na penzi la Rayavanny ambaye hajawahi kuhusishwa na mwana dada yeyote. Kila la Kheri wakali wetu na tusubirie Perfect Combo.
No comments:
Post a Comment