Wanafunzi Wakumbwa na Ugonjwa wa Kuanguka Ovyo Ovyo - FARMERCIST 254

FARMERCIST 254

This site discusses farming issues in relation to Kenya with particular emphasis on poultry farming.

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 16 November 2016

Wanafunzi Wakumbwa na Ugonjwa wa Kuanguka Ovyo Ovyo

Wanafunzi wa kike 12 wanaosoma Shule ya Msingi Nditi, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, wamekumbwa na ugonjwa wa kuanguka ghafla na wengine kupoteza fahamu, walipokuwa wakicheza katika viwanja vya shule hiyo. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Amon Livigha, alikiri kutokea tukio hilo katikati ya wiki iliyopita, saa mbili asubuhi. Alisema baada ya tukio hilo, baadhi ya wazazi walifika shuleni hapo na kuwachukua watoto wao na kwenda nao nyumbani. “Nilipata taarifa ya kuanguka kwa wanafunzi hao nikiwa darasani nafundisha, hivyo kutokana na uzito wa tatizo, nililazimika kukatisha masomo na kwenda kuwahudumia watoto hao. “Wakati tukiendelea kufanya utaratibu wa kuwakimbiza wanafunzi hao kituo cha afya kupatiwa huduma, baadhi ya wazazi walikataa watoto wao wasipelekwe hospitali na kuondoka nao,” alisema. Mwalimu Livigha alisema kutokana na tukio hilo, kamati ya shule, wazazi na uongozi wa Serikali ya kijiji na kata hiyo wamekutana kujadili suala hilo. Mtendaji wa kata hiyo, Juma Mng’anga, alikiri kutokea tukio hilo na kueleza kuwa tayari wameshatoa taarifa makao makuu ya wilaya, Nachingwea.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages